Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mhe. Raymond Stephen Mwangwala amewasihi wananchi wilayani hapa kuiunga mkono serikali kwani imesogeza huduma za kijamii karibu na wananchi wilayani Ngorongoro ili kuwapunguzia adha ya kufuata huduma mbali.
Ameyasema hayo ijumaa ya tar 25/8/2023 wakati akitembelea na kukagua miradi ya afya,elimu na miundombinu ya barabara inayotekelezwa na serikali kuu pamoja na wadau wa maendeleo ambapo amewasihi wananchi kushiriki kwa kulinda miundombinu hiyo na ubora wake na wazazi kuwapele watoto wote shule na wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya kwani shule na vituo vya afya vinajengwa na kumafikika kupitia miundombinu ya barabara ambayo pia imeboreshwa,huku akiwaagiza wakandarasi kuzingatia vipimo na ubora wakati wa ujenzi.
Kwa upande wake Julius Fanuel mshauri ufundi wa nyanda za malisho na maisha kutoka Frankfut Zoological Society ofisi za Loliondo amesema miradi wanayoitekeleza chini ya mradi wa maendeleo ya ikolojia ya Serengeti ukiwa na lengo la kupunguza msukumo wa wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi za taifa ambao unafadhiriwa na Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani kupitia benki ya watu wa ujerumani yani KFW pamoja na frunkfult zoological society.
Naye Nkunzi james Nyabakari mhandisi miundo ujenzi kutoka kampuni ya Osaka Construction Ltd kwa niaba ya wajenzi wa miradi hio amesema wanajenga majengo 18 katika vijiji 16 ambavyo ni Ngarwa,Nan,Sakala,Mondorosi,Sero,Enguserosambu,Oloipiri,Lemishiri Magaiduru,olorien Magaiduru,Mageri,Samunge,Ngobereti,Arash,Ormanie na Olalaa.
Miradi iliyo kaguliwa na Mhe. Mwangwala ni barabara ya kipambi,madarasa mawili shule ya lopolun,shule ya njoriet,shule tarajali ya kirtalo mbopong losirw ambayo itatapisha shule ya kirtalo yenye wanafunzi zaidi ya elfu moja(1,000) madarasa ya mradi wa bust shule ya msingi Ololosokwani ,Ololosokwan sekondari,ujenzi wa nyumba ya watumishi kituo cha afya sero,barabara ya KFW Mairowa-Njoroi,zahanati ya Njoroi,zahanati ya mondorosi na madarasa katika shule ya msingi Sukenya.
.......End......
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.