• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhamira
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji na Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Kata
      • Loliondo
        • Ololosokwan
        • Soitsambu
        • Enguserosambu
        • Maalon
        • Oloirien Magaiduru
        • Piyaya
        • Orgosorok
        • Oloipir
        • Arash
      • Ngorongoro
        • Alailelai
        • Naiyobi
        • Olbalbal
        • Nainokanoka
        • Kakesio
        • Ngorongoro
        • Eyasi
        • Endulen
        • Ngoile
        • Alaitolei
        • Misigyo
      • Sale
        • Sale
        • Malambo
        • Digodigo
        • Oldonyosambu
        • Samunge
        • Pinyinyi
        • Kirangi
        • Engaresero
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezw
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

UFAHAMU UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Posted on: January 15th, 2024


Na Mpoki Daudi Mwangomale -AFISA AFYA MAZINGIRA


Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “ *Vibrio cholera* ”.


*CHANZO CHA UGONJWA*


• Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu.


• Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi cha mtu bila yeye binafsi kuonyesha dalili zozote za ugonjwa.


*DALILI ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.*


Mgonjwa wa Kipindupindu huwa na dalili zifuatazo:


• Kuharisha mfululizo au mara kwa mara bila tumbo kuuma ambako kunaweza kuambatana na kutapika.


• Kinyesi au matapishi huwa ya maji maji yasiyo na harufu, yanayofanana na maji yaliyooshewa mchele.


• Kusikia kiu sana, macho kudidimia na ngozi kusinyaa ambavyo hutokana na upungufu wa maji mwilini.


• Kuishiwa nguvu, kuhema haraka haraka na kulegea. Hali hii hutokana na upungufu wa maji na madini mwilini.


*KIPINDUPINDU KINAVYOENEA.*


• Kula chakula au kunywa kinywaji chochote kilicho na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa mfano:-


. Kunywa maji yasiyochemshwa.


- Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira ambayo siyo safi.


- Kula matunda yasiyooshwa kwa maji safi na salama.


- Kunywa pombe za kienyeji zilizoandaliwa katika mazingira machafu au kunywea katika vyombo vichafu.


- Kula mboga za majani, kachumbari na saladi bila kupikwa au kuziosha kwa maji safi na salama.


• Kula chakula au kumlisha mtoto bila kunawa mikono kwa sabuni na maji safi na salama yanayo tiririka.


• Kuosha au kuhudumia mwili wa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa kipindupindu bila kujikinga.


• Kunawa mikono kwenye chombo kimoja kwa mfano ndani ya bakuli au beseni kabla ya kula chakula.


• Kutotumia choo au utupaji ovyo wa kinyesi.


• Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni.


• Kuweka mazingira katika hali ya uchafu mfano kutupa taka ovyo bila kuzingatia kanuni za afya.


• Kula vyakula vilivyopoa na visivyofunikwa.


• Kutiririsha maji ya chooni ardhini na hivyo kusababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji na chakula.


· Inzi huchangia kueneza ugonjwa wa kipindupindu kwa tabia zake za kutua chooni kwenye

kinyesi, uchafu na hata vyakula na vinywaji.


*MADHARA YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU*


• Hofu miongoni mwa jamii katika sehemu yenye mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.


• Kifo kutokana na ukosefu wa maji na madini mwilini baada ya kuharisha na kutapika sana.


• Kushuka kwa uchumi kutokana na familia/jamii kuacha shughuli za uzalishaji mali ili kumuhudumia mgonjwa na kushiriki katika misiba.


• Serikali hutumia fedha nyingi kwa ajili ya dawa, posho kwa watumishi katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.


*JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU*


• Kujenga choo bora na kukitumia Ipasavyo


• Kufunika tundu la choo na kufunga mlango baada ya matumizi yake.


• Kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni baada ya:.


- kutumia choo.


- kumtawaza mtoto na kabla ya kula au kumlisha mtoto.


• Kula chakula kikiwa bado moto na kufunika chakula kilichoandaliwa tayari kwa kuliwa.


• Kunywa majiyaliyochemshwa na kuhifadhiwa katika chombo kisafi na salama.


• Kusafisha vyakula vinavyoliwa vibichi (kama vile matunda na mboga) kwa kutumia maji safi na salama yanayotiririka.


• Kuhakikisha usafi wa mazingira ya vilabu/baa, wahudumu na vyombo vitumikavyo. Pombe za kienyeji ziandaliwe kwa maji yaliyochemshwa.


• Weka mazingira katika hali ya usafi.


· Kumbuka, kuchuja maji yaliyochemshwa kunaweza kuchafua maji kwa kuingiza

vimelea.Hivyo, chuja maji kabla ya kuyachemsha.


*KUHUDUMIA MGONJWA WA KIPINDUPINDU*


- Mgonjwa wa kipindupindu hupoteza maji mengi na madini muhimu mwilini anapoharisha na

kutapika. Ili kuokoa maisha ya mgonjwa ni muhimu kuchukua hatua zifuatazo:


• Mpe mgonjwa dawa ya mchanganyiko wa sukari na chumvi(ORS), maji, uji mwepesi, supu nk. mara kwa mara.


• Mpeleke mgonjwa haraka iwezekanavyo katika kituo cha afya/zahanati/ hospitali au kituo cha kutibu kipindupindu kilicho karibu nawe.


• Matapishi na kinyesi cha mgonjwa ni hatari kwa afya yako. Kwa hiyo nguo na vitu vingine vilivyochafuliwa na mgonjwa vilowekwe kwenye kemikali maalumu (mfano Jik) au vichemshwe

ili kuua vimelea vya kipindupindu na kasha visafishwe kwa sabuni.


• Ndugu waliokuwa wakiishi na mgonjwa au wale wanaomhudumia wahakikishe wanapata

dawa za kinga dhidi ya kipindupindu.


*Angalizo:*


- Ni lazima wakati wote kuwa msafi ili kuzuia vimelea vya ugonjwa visiingie kinywani kwako kwa njia zilizotajwa hapo juu.


*Tahadhari:*


- Maiti ya mgonjwa wa kipindupindu ni hatari, usijishughulishe na kuosha maiti hiyo bali izikwe

haraka kwa kufuatwa ushauri wa wataalam wa afya.

Matangazo

  • TANGAZO LA RATIBA YA UCHAGUZI NA UANDIKISHAJI WA UCHAGUZI. September 26, 2024
  • TANGAZO LA UANDIKISHAJI VIJANA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. October 01, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI.2. September 29, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI. September 29, 2024
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • WILAYA YA NGORONGORO YAPONGEZWA KWA UKUSANYAJI WA ΜΑΡΑΤΟ ΝA KUPATA HATI SAFI.

    June 11, 2025
  • NGORONGORO YANG'ARA MASHINDANO YA RIADHA UMITASHUMTA MKOA 2025.

    June 03, 2025
  • KAMPENI YA KITAIFA YA UTOAJI CHANJO NA DAWA KINGA ZA MAGOJWA YA MINYOO NA TRAKOMA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGORONGORO.

    May 30, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPONGEZA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI WILAYANI NGORONGORO

    May 16, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Afisa kilimo Ngorongoro aeleza na kufafanua namna ya kupata mazao yenye afya na mbegu bora kutumia katika kilimo.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Upimaji darasa la Nne 2019
  • Taarifa na Matangazo
  • Mikataba na Miongozo
  • machapisho mbalimbali
  • Habari kwa umma
  • Taarifa kwa Umma
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019.
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NGORONGORO

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Rais
  • Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
  • NGORONGORO DC YOUTUBE CHANEL
  • MATOKEO YA UPIMAJI DARASA LA NNE 2019 WILAYA YA NGORONGORO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.