Ngorongoro, Arusha
Jumatatu 27,November 2018
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Mgufuli kupitia Wizara ya Wazee jinsia na watoto imetoa shilingi milioni mianne 400 kwa kata ya Osinoni iliopo tarafa ya Ngorongoro Wilaya ya Ngorongoro ili kujenga kituo cha Afya.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Wilaya Ngorongoro Bw.Rafael Siumbu alipotembelea kata hiyo ili kushuhudia ujenzi unaoendelea ambapo ametaja kufurahishwa na kazi inayoendelea na wananchi wa eneo hilo kujitolea kufanya kazi inayowahusu ili kukamilisha kazi ya ujenzi hiyo.
Hata hivyo amesema pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta maendeleo,kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya Afya vinavyojengwa Tanzania nzima na serikali ya Awamu ya Tano pamoja na hayo Bw Raphael Siumbu amesema kandarasi anayejenga kituo hicho amehaidi kukabidhi kituo hicho fikapo tarehe 7 January 2019, nakutoa wito kwa wanachi wanaojengewa vituo hivyo kote kutoa ushirikiano ili kukamilisha kazi hizo mapema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ngorongoro na Diwani wa kata ya Arash Mh.Mathew Siloma ameshukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutoa shilingi milioni 400 ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho na kusema kuwa halmashauri ya wilaya Ngorongoro wameshatoa shilingi milioni thelathini ili kuunga mikono juhudi za serikali za kutaka kujenga jengo la OPD na kutoa rai kwa kamati husika ili kusimamia na kuzingatia ubora wa ujenzi wa kituo hicho.
Naye mjumbe wa kamati ya ujenzi katika kituo hicho na diwani wa kata ya Endulen Mh Emanuel Shangai amesema kuwa ameridhika na kazi inayofanywa na kandarasi na kamati itaendelea kushughulikia changamoto zilizopo ili kazi hiyo ikamilike kwa Wakati.
Imetolewa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Moja ya majengo ya kituo cha afya Osinoni likiwa katika hatua ya msingi
Nyumba ya Mganga ikiwa katika hatua ya lenta kwenye ujenzi wa kituo cha afya Osinoni
Mweyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango Mh.Methew Siloma(Diwani kata ya Arash) akikoroga zege kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Osinoni wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi Huo
Makamu Mweyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango Emanuel Shangai(Diwani kata ya Arash) akikoroga zege kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Osinoni wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi Huo
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.