Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Mohamed Bayo ameambatana na Ndugu Abubakar Gati Katibu Mkuu CCM Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Bw. Emmanuel Sukumus, Afisa Elimu Sekondari Wilaya pamoja na viongozi wa Divisheni mbalimbali ikiwemo Divisheni ya maendeleo ya jamii na Divisheni ardhi katika kukagua eneo la kujenga Sekondari mpya katika eneo la kijiji cha Sitet kilichopo Kata ya Maalon
Aidha ukaguzi wa eneo hilo umehusisha makubaliano na maridhiano ya ujenzi wa shule hiyo baina ya Serikali na Viongozi wa eneo hilo. Ambapo Diwani wa kata hiyo Mhe. Damian Rago ameongoza zoezi la upimaji wa eneo hilo, pia amesema wananchi wapo tayari kutoa ushirikiano katika ujenzi wa Shule hiyo.
"Sisi kama wanakijiji tutahakikisha tunatoa ushirikiano wowote utaohitajika pia mahitaji ya ujenzi kama mchanga na mawe vipo Karibu na eneo hili hivyo itarahisisha ujenzi, pia tunapenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea miradi mingi ya maendeleo hapa Wilayani kwetu". amesema Mhe. Damian.
Hata hivyo Afisa Elimu Sekondari amewapongeza viongozi wa kata ya Maalon Kwa kuchagua eneo lenye sifa stahiki kwa ujenzi wa Sekondari hiyo mpya, pia amewaasa viongozi wa kata hiyo kuepuka migogoro ili kazi hiyo ifanyike Kwa ufanisi
"Niwapongeze kwa kuchagua eneo zuri la kujenga Sekondari, mradi huu wa uboreshaji wa Shule za Sekondari utaenda kuwanufaisha Wananchi wa eneo hili hivyo muwashirikishe wananchi kikamilifu pia niwaase viongozi kuepuka migogoro na mivutano yeyote kwani itakwamisha zoezi hili kufanyika ipasavyo" amesema Bw. Sukumus
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya ngorongoro Mhe. Mohamed Bayo amewapongeza Viongozi wa kata hiyo Kwa kuonesha juhudi za maendeleo
Hata hivyo Mhe. Bayo amefikisha salamu kutoka Kwa Mbunge wa Wilaya ya ngorongoro kuwa Mhe. Mbunge amewaomba wananchi wa eneo hilo kuonesha ushirikiano ili zoezi hilo lifanyike Kwa haraka.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngorongoro amesifu jitihada za viongozi Kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita wa kutambua umuhimu wa Elimu katika jamii pia amewashauri wananchi wa kata hiyo kuwapa viongozi ushirikiano.
"Niwapongeze Kwa kutambua jitihada za kuboresha elimu katika wilaya yetu pia niwashauri kutoa ushirikiano Kwa viongozi ili Jambo hili lifanikiwe pia viongozi ni wakati wakuitisha mikutano na wananchi ili kuondoa mivutano na kuongeza ushirikiano" amesema Ndg. Abubakar Gati
Wananchi wa kijiji cha Sitet kimetoa eneo lenye ukubwa wa Hekari 55.6 kwaajili ya ujenzi wa Sekondari mpya inayotarajiwa kuaanza kujengwa hivi karibuni.
Ikumbukwe kuwa jitihada zote za maendeleo na miradi ya maboresho Wilayani ngorongoro inafanyika kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 chini ya Dk.Samia Suluhu Hassan.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.