Ngorongoro, Arusha
Jumanne 27,November 2018
Mheshimiwa Rashid Mfaume Taka Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro ameongoza viongozi wa mtandao wa wajane Tanzania(Mkurugenzi wa mtandao wa wajane Taifa mama Rose Sarwat ) pamoja na viongozi mbalimbali wa mtandao huo wilayani Ngorongoro bila kumsahau Afisa maendeleo ya jamii Ndugu Thomas Nade,mwakilishi Baraza la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha Ndugu Elizabeth Gibaseya ,watendaji,waratibu Elimu na viongozi wa mila na wananchi katika uzinduzi wa katiba ya vikundi 20 vya mtandao wa wajane Kata ya Malambo na kuwapatia vyeti,kuzindua kibao cha mtandao wa wajane lakini pia amefanikiwa kuendesha harambee ndogo kwa ajili ya kina mama hao ambapo kiasi cha shilingi za kitanzania laki tisa zilipatikana
Wajane wana haki sawa na watu wengine hivyo wanahitaji kutambuliwa na serikali,vyama vya kisiasa na kila mdau wa maendeleo ndani ya jamii ili waweze kufikia malengo yao likiwemo jukumu zito la kulea familia ambazo wameachiwa na wenza wao ambao wametangulia mbele ya haki.
Imetolewa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka akikabidhi katiba kwa moja ya viongozi wa vikundi vya mtandao wa wajane kata ya Malambo
Afisa Maendeleo ya Jamii Bw.Thomas Nade akishirikiana na Elizabeth Gibaseya wakihesabu fedha zilizochangwa baada ya harambee kuendeshwa katika uzinduzi wa katiba ya vikundi 20 vya mtandao wa wajane kata ya Malambo
kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi katiba ya vikundi 20 vya mtandao wa wajane
Mwenyekiti wa Kijiji cha Malambo akikabidhi mchango wake katika harambee iliyoendeshwa kuwachangia mtandao wa akinamama wajane kata ya Malambo
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro akizindua kibao cha mtandao wa wajane katika kata ya malambo
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.