Wananchi wajasiriamali kupitia makundi wanawake, vijana na wenye ulemavu wamehimizwa kuchangamkia fursa na kuchukua mikopo isiyokuwa na riba, inayotolewa na Serikali kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri zao.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.Kenani Laban Kihongosi alipokutana na wakazi wa Arusha kwa makundi ya wafanyakazi na wamiliki wa saluni pamoja na kundi la waendesha bodabodada, bajaji na maguta, Jijini Arusha Julai 22,2025.
Mhe.Kihongosi amesema kuwa, Serikali imetoa fursa hiyo ili kuwawezesha wananchi wajasiriamali wasio na uwezo na sifa za kukopesheka kwenye taasisi nyingine za kifedha ili waweze kukuza mitaji yao ya biashara sambamba na kujikwamua kikuchumi hivyo ni wakati wao wa kuchangamkia fursa hiyo.
Ametoa mfano wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambalo tayari lina shilingi Bilioni 5.5 kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali wenye sifa kwa makundi hayo na kuwasisitiza kujiunga kwenye vikundi na kwenda kupata fedha hizo ambazo Serikali imetenge kwa ajili yao.
"Jamani ndugu zangu msiogope, hapa Jiji la Arusha kuna shilingi Bilioni 5.5, tumieni fursa hii adhimu, nendeni mkakope fedha zisizo na riba, fedha ambazo masharti yake sio magumu kama ilivyo kwa Taasisi za kifedha, fuateni taratibu mpate fedha zipo kwa ajili yenu" Ameweka wazi Mhe.Kihongosi
Hata hivyo, amewasisitiza wajasiriamali hao, kufanya biashara zao huku wakiwa na malengo ya maendeleo na sio kutumia pesa zao vibaya na kuishia kwenye majuto na kulalamika, kwa kuwa unapoweza kutunza kidogo unachopata ni rahisi kijifanyia shughuli za maendeleo kutokana na kidogo kinachopatikana.
"Pesa unayopata hakikisha unaipangilia na kuitumia vizuri, hakuna pesa ndogo, hicho hicho kidogo kipangilie na kukitumia vizuri, wenye mafanikio huanzia chini, kama vijana msitamani maisha ya wengine, riziki unayoipata ndio Mungu amekupangia jipange kupambana na maisha kwa fedhq hiyo unayoipata kupitia biashara yako hiyo hiyo unayoiita ndogo" Ameshuri Mhe. Kihongosi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.