Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela amewataka wakufunzi 399 wa zoezi la sensa ngazi ya Mkoa toka Wilaya 7 za Mkoa huo kuwa waadilifu,
Wazalendo na wenye weledi mkubwa wakati wa utekelezaji wa jukumu la kutoa mafunzo ngazi za Wilaya na Halmashauri.
Mongela amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya wakufunzi hao yalioanza tarehe 06 Julai 2022 na kudumu kwa siku 21 ambapo amebainisha zoezi la Sensa kuwa zoezi nyeti na la kizalendo lenye kuiwezesha Serikali kupata takwimu muhimu za kupanga mipango ya maendeleo " niwatake mkatekeleze jukumu la kufundisha kwa uadilifu mkubwa, uzalendo na kwa weledi mkubwa "amehimiza Mongela
Vilevile Mhe.Mongela amesema ni muhimu zoezi la Sensa kutekelezwa kwa umakini na uimara kwani takwimu za Sensa zitasaidia kwa mapana azma ya Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe.,Rais Samia Suluhu Hassan kupanga mipango ya kuwaletea wananchi wake maendeleo .
Mafunzo hayo ya wakufunzi ngazi ya Mkoa yamefungwa katika ukumbi wa Chuo cha Uasibu Njiro ikiwa ni hatua katika utelelezaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe 23 Agusti 2022
SENSA KWA MAENDELEO ,JIANDAE KUHESABIWA
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.