Jumla ya Wanafunzi 576 wa kidato Cha sita Wilayani Ngorongoro wameanza kufanya mtihani wao wa Taifa wa elimu ya upili wa juu leo tarehe 5 Mei, 2025.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ina jumla ya shule 6 za Sekondari ya elimu ya upili wa juu (kidato cha tano na sita) zenye idadi ya Watahiniwa 576 kwa ujumla wake ambapo Watahiniwa wa jinsi ke wakiwa 283 na jinsi me wakiwa 293
Afisa Elimu Sekondari Mwl. Emmanuel Sukums amesema divisheni ya elimu sekondari imejipanga vizuri kwa muda wote wa kuanza kwa zoezi hili la mtihani mpaka litakapomalizika Pia, amewatakiwa mtihani mwema watahiniwa wote wilayani hapa.
Mkurugenzi Mtendaji Bw. Murtallah S. Mbillu kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anawatakia kila la kheri na mtihani mwema Watahiniwa wote wa kidato cha sita mwaka 2025 hapa nchini.
Aidha, Bw. Murtallah wiki iliyopita ya tarehe 25 Aprili, 2025 alitembelea shule ya Sekondari Embarway tarafa ya Ngorongoro wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika tarafa hiyo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.