Wananchi Wilaya ya Ngorongoro na Watumishi wa umma wameungana kwa pamoja wameungana kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara kujitokeza kufanya usafi katika eneo jipya la soko la Wasso, kupanda miti katika eneo la Shule ya Msingi Wasso.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Kanali Wilson Sakulo ambapo shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji miche ya miti 150, usafi wa mazingira, upimaji afya wa hiari, hali ya lishe pamoja na uchangiaji damu wa hiari ambayo imeenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Changia damu, Okoa Maisha".
Aidha Mkuu wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa fursa ya kila Wilaya kuadhimisha siku hiyo wakiwa katika maeneo yao .
" Pamoja na kusherehekea maadhimishi haya tumepata elimu ya ya masuala ya lishe, hivyo niwapongeze kwa moyo mkunjufu kujitokeza na kushiriki maadhimisho haya ya uhuru wa Tanzania Bara sisi tumeitendea haki" amesema Mhe. Kanali Sakulo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.