Watoto wenye umri wa miaka 5 hadi 14 wilaya ya ngorongoro wameanza kupatiwa dawa za kuua na kuzuia minyoo ya tumbo (tiba kinga) tarehe 19/04/2018. Huu ni mpango wa serikali wa kuwakinga watoto na didhi ya minyoo ya tumbo. Zoezi hili linaendeshwa kwa muda wa siku mbili kwa wanafunzi wenye umri lengwa wa shule zote za msingi wilayani Ngorongoro.
Mgeni rasmi katika zoezi hili alikuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Emmanuel Sukums akiambatana na wageni wengine akiwemo Kaimu Mkuu wa Wilaya Ngorongoro ndugu William Ndossi, kaimu Afisa Elimu Msingi Mwalimu Seraphine A. Kangu na Kaimu mganga mkuu Dr. Wipyana Mkumbwa.
Katika zoezi hilo Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wilaya Dokta Nestory Mkenda na mwakilishi wa Wizara ya Afya Dokta Mgalula walitoa elimu juu ya jinsi minyoo inavyoenea, madhara na namna ya kujikinga na minyoo ya tumbo.
Uzinduzi wa zoezi la utoaji dawa za minyoo kiwilaya ulifanyika katika shule ya msingi Wasso ambapo wanafunzi wengi walijitokeza na kumeza dawa hizo.
Mgeni rasmi alizindua zoezi kwa kuwapa washiriki dawa kwa kuanzia na wanafunzi wawakilishi 4, wageni waalikwa, walimu na wafanyakazi wengine
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.