Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro Bwana Raphael John Siumbu amewaasa baadhi ya watumishi wa Halmashauri kuepuka kufanya kazi kwa mazoea. Hayo yalijiri siku ya Tarehe 30 June 2017 wakati alipokutana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kukumbushana wajibu na majukumu ya kila Mtumishi.
Bwana Siumbu alisisitiza kuwa kila mtumishi atimize majukumu na wajibu wake kwa wakati na kuhakikisha kuwa watumishi wanawahi katika vituo vya kazi na kuwepo katika kituo cha kazi muda wote wa kazi.
Bwana Siumbu aliagiza kuwa kila mtumishi ajaze fomu ya OPRAS na kumuagiza Afisa Utumishi Bi. Hadija Mkumbwa kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha kuwa fomu hizo zinajazwa ipasavyo na kwa wakati. Bi Hadija Mkumbwa alitoa maelekezo machache kuhusu ujazaji wa fomu Hizo za OPRAS na kuagiza kuwa wiki hii inayoanza itakuwa ni wiki ya OPRAS hivyo kwa pamoja kuhakikisha watumishi wanatimiza agizo hilo. Pia alitaka kila Idara na Kitengo kuhakikisha kunakuwa na mpango kazi wa wiki na mwezi kutoka katika Mpangokazi wa Idara au Kitengo wa Mwaka.
Pamoja na mambo mengine, Bwana Siumbu alisema haridhishwi na kazi za barabara zinazoendelea katika Wilaya na kumtaka Mhandisi wa Ujenzi Bwana Msetu Naidye kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara. Bwana Siumbu alisema hayo baada ya Kukagua kazi za ujenzi wa Barabara zinazoendelea katika Wilaya.
Maagizo hayo yalitolewa kwa watumishi wote wa Wilaya Ngorongoro kupitia kikao hicho
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.