WAWEZESHAJI WA TASAF KATIKA HALMASHAURI YA NGORONGORO WAJENGEWA UWEZO KUTOA ELIMU KATIKA VIKUNDI
Kaimu Mkurugenzi Mtendajiwa wa Halmashauri ya Ngorongoro,Ndg Peter Juma amewataka wawezeshaji wa mfuko wa kunusuru kaya maskini (TASAF) katika Halmashuri hiyo kutumia vyema mafunzo wanayopewa ya utunzaji wa kumbukumbu na fedha kuvifundisha vikundi vya wananchi wanaofadhiliwa TASAF ili waweze kujiinua kiuchumi kutumia kupitia fedha wanazopewa katika kubuni na kuanzisha miradi ya uzalishajimali.
Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 5 ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa TASAF Ngazi ya Wilaya na Kata katika Halmashauri hiyo ambapo amewataka kutumia mafunzo hayo kama chachu ya kwenda kutoa elimu katika vikundi vya jamii husika vinavyo toka katika kaya maskini ili viweze kuongeza kipato na kupiga hatua kiuchumi.
Mtaalamu wa Mafunzo na Ushirikishwaji kutoka TASAF Makao makuu,Ndg.Rashid Mchata amesema wawezeshaji kwenye Halmashuri zote nchini wamechangia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa TASAF kuwa rahisi ,hivyo ametoa rai kwao kutumia mafunzo hayo kuisaidia jamii kujua kutunza kumbukumbu na kuweka akiba kwa lengo la kujikwamua kutoka hali duni.
Mratibu wa TASAF katika Halmashuri hiyo Zablon Kitandu amesema vijiji 31 kati 72 vya Halmashauri hiyo vipo katika mpango wa kunusuru kaya masikini vyenye jumla ya vikundi 221 .vyenye wanachama 2931 kati yao wanawake ni 2898 vimeundwa na vinajiendesha ..
Aidha Zablon amesema vikundi hivyo vinajiendesha vyenyewe na vimeshapewa shajala mbalimbali likiwemo daftari la kutunza kumbukumbu na sanduku la kuhifadhia nyaraka mbalimbali vikundi hivyo vinahitaji mafuzo ili viboreshe utendaji .
Baadhi ya wawezeshaji wanaopata mafunzo hayo Godwine Mtune,Merry Mhando wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kuwajengea uwezo wa kwenda kuwafundisha wanavikundi walioko katika maeneo yao kutumia fedha wanazopata kujikwamua katika umaskini.
Mafunzo hayo ya TASAF ambayo yanafanyika katika mikoa miwili tu Nchini ,ambapo kwa mkoa wa Njombe yamekamilika na kwa Mkoa wa Arusha Arusha yanaendelea,na kwa Halmashauri ya Ngorongoro yanafanyika katika kumbi za Halmashauri .
Bw.ALLEN MWAMBOLA mshiriki katika mafunzo akiwa makini kumsilizia mwezeshaji
Mwezeshaji kutoka makao makuu Bw.Rahid Mchata akitoa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya wilaya na kata
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.