• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhamira
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji na Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Kata
      • Loliondo
        • Ololosokwan
        • Soitsambu
        • Enguserosambu
        • Maalon
        • Oloirien Magaiduru
        • Piyaya
        • Orgosorok
        • Oloipir
        • Arash
      • Ngorongoro
        • Alailelai
        • Naiyobi
        • Olbalbal
        • Nainokanoka
        • Kakesio
        • Ngorongoro
        • Eyasi
        • Endulen
        • Ngoile
        • Alaitolei
        • Misigyo
      • Sale
        • Sale
        • Malambo
        • Digodigo
        • Oldonyosambu
        • Samunge
        • Pinyinyi
        • Kirangi
        • Engaresero
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezw
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

WAZIRI MCHENGERWA "SIKU ZA WATUMISHI WABADHIRIFU ZINAHESABIKA"

Posted on: November 6th, 2023

OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewatahadharisha viongozi katika Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambao ni wazembe, wasio na nidhamu na wabadhilifu kuwa siku zao zinahesabika.


Akichangia hoja ya taarifa za kamati tatu za Bunge kuhusu ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) Mchengerwa alisema:" wale wote waliotajwa kwenye ripoti naomba kusema maneno yafuatayo; ole wake kiongozi yeyote mzembe, asiye na nidhamu na mbadhilifu  kwenye wizara yangu na nitakayemkuta huko naomba niwaambie siku zao zinahesabika."Kauli ya Mchengerwa iliamsha shangwe kutoka kwa Wabunge huku wakigonga meza.

Aidha, Mchengerwa alimuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Adolf Nduguru kuchukua hatua dhidi ya Mkurugenzi wa Igunga ambaye alikua Mkurugenzi Kigoma Manispaa, Athuman Msabila kumsimamisha kazi mara moja kwasababu ya ushiriki wake wa fedha za mifumo akishirikiana na watendaji wa mifumo walioko Ofisi ya Rais Tamisemi waliotajwa.


 "Watu hawa wasimamishwe kazi mara moja."


Aidha, Mchengerwa amesema tayari wizara yake imeanza kutekeleza taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG kwa kuchukua hatua mbalimbali kwa wakurugenzi wa halmashauri zikiwemo za kuwasimamisha kazi, kutengua uteuzi na kuwafikisha mahakamani.


" Serikali ya awamu ya sita inachukia hatua madhubuti za kupambana na wabadhilifu wa fedha za umma kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa."

Amesema wamewasimamiasha kazi watumishi walioshiriki kwenye ubadhirifu wa fedha za Serikali katika Halmashauri mbalimbali na kuchukua hatua kwa wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali ikiwemo wa Jiji la Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam na Arusha.


"Na hata aliyekuwa Mkurugenzi wa Sumbawanga akahamishiwa kwengine tumemrejesha ili akajibu kesi iliyoko mahakamani. Zile taarifa kuwa kuna watu wanahamishwa, katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita ya Dk.Samia Suluhu Hassan mtumishi yeyote popote alipo awe amehamishwa, awe amestaafu, atakayeshiriki kwenye ubadhilifu wa fedha za umma hatutasita kumchukulia hatua na huo ujumbe tumeshautuma."


"Hapa tunavyozungumza wataalam wangu wako uwandani kuchunguza taarifa ambazo tumeendelea kuzipokea kutoka kwa watoa taarifa mbalimbali. Kwa Sasa tunaendelea na uchunguzi katika Halmashauri za Kibaha, Kigoma, Uvinza, Ileje na Ifakara."


Alisema pia wameshachukua hatua ya kuwaondoa wakuu wa vitengo vya manunuzi na ugavi 23, wahasibu 16, wakuu wa vitengo vya rasilimali watu 6 na wakaguzi wa ndani wawili, waganga wakuu wa mikoa 10 na waganga wa Wilaya 46.


"Taarifa hii ya LAAC iwe kengele ya kutuamsha kila mmoja tutahakikishe tunawatendea haki watanzania. Serikali inafanya kazi kubwa sana ni lazima tumtendee haki Mheshimiwa Rais kwa sisi viongozi kufanyakazi kwa bidii kila mmoja katika eneo lake."


"Wabunge wasisite kubainisha popote wanapoona changamoto, Tamisemi tutakuwa nanyi Leo na kesho kuhakikisha tunafanya kazi kwa ajili ya Watanzania."

Matangazo

  • TANGAZO LA RATIBA YA UCHAGUZI NA UANDIKISHAJI WA UCHAGUZI. September 26, 2024
  • TANGAZO LA UANDIKISHAJI VIJANA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. October 01, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI.2. September 29, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI. September 29, 2024
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • NGORONGORO MSTARI WA MBELE KUHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

    May 09, 2025
  • KISIMA CHA MAJI SAFI KUCHIMBWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA NGORONGORO

    April 25, 2025
  • ZIARA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI TARAFA YA NGORONGORO.

    April 28, 2025
  • WANAFUNZI 576 WA KIDATO CHA SITA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA NGORONGORO.

    May 06, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Afisa kilimo Ngorongoro aeleza na kufafanua namna ya kupata mazao yenye afya na mbegu bora kutumia katika kilimo.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Upimaji darasa la Nne 2019
  • Taarifa na Matangazo
  • Mikataba na Miongozo
  • machapisho mbalimbali
  • Habari kwa umma
  • Taarifa kwa Umma
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019.
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NGORONGORO

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Rais
  • Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
  • NGORONGORO DC YOUTUBE CHANEL
  • MATOKEO YA UPIMAJI DARASA LA NNE 2019 WILAYA YA NGORONGORO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.