"Tulikua na Vituo vya Afya 38 ambavyo vyote vilitumika kutoa huduma ya chanjo, tumetekeleza zoezi kwa asilimia 136, tulipata jumla ya dozi 54, 020 tunaishukuru Wizara ya Afya kwa kutoa chanjo pamoja na fedha kwajili ya utekelezaji wa zoezi la utoaji chanjo"-Mratibu wa chanjo Wilaya ya
Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuipitia Wataalamu wake ilianza rasmi zoezi la utoaji chanjo ya Surua na Rubella kuanzia tarehe 15-19 Februari, 2024 kwa Watoto wote waliyochini ya miaka mitano, mpaka kufikia tarehe Februari 19 siku ya mwisho ya zoezi jumla ya watoto 50, 709 walifikiwa na kupatiwa chanjo ambapo ni sawa asilimia 136 zaidi ya lengo lilikusudiwa ikiwa kusudi ilikua ni kuchanja Watoto 37, 364 sawa na asilimia 100
Hata hivyo Mratibu wa chanjo Wilaya ya Ngorongoro Bw. Thomas Nchimbi amesema sababu iliyochangia kuvuka lengo tulilojiwekea ni kutokana na uhamasishaji uliyofanywa kwa Wananchi pamoja na ushiriakiano uliyotolewa na vyombo habari kama Loliondo fm, viongozi wote wa Serikali na Viongozi wa kidini wa Wilaya ya Ngorongoro
"tuna Vituo vya Afya 38 ambavyo vyote vilitumika kutoa chanjo wakati wote kwa siku nzima, tulikua na vituo vya muda 154 (kliniki ya mkoba) ambapo Wahudumu wa Afya walikwenda maeneo tofauti kutoa huduma ya chanjo pia tulikua na maeneo maalumu 5 kama Shule ambayo tuliyatumia ili kuwasogelea Wananchi na kutoa chanjo kwa Watoto kusudiwa, tunashukuru muitikio kwa Wananchi ulikua mkubwa sana" amesema Nchimbi
Aidha Bw. Nchimbi richa ya kufanikiwa katika zoezi zima la utoaji chanjo, Sekta ya Afya ilifanikiwa kujua kuna kundi la Watoto 136 halikuwahi kupata chanjo ya aina yoyote katika kipindi chote cha maisha mpaka walipofikiwa, hivyo walipewa chanjo ya Surua na utaratibu wa kuwapa chanjo zingine ambazo hawakuwahi kupata zilifanyika ili kusaidia kuimarisha kinga zao za mwili
Kwa niaba ya Divisheni ya Afya Bw. Thomas Nchimbi ametoa pongezi na Shukrani kwa Wizara ya Afya kwa kutoa chanjo ambapo Wilaya ya Ngorongoro pekee ilipokea dozi 54, 020 za chanjo
"tunaishukuru Wizara ya Afya inayoongozwa na Mhe. Ummy Mwalimu kutupatia dozi za chanjo pamoja na fedha za kutosha kwaajili ya kutekeleza na kukamilisha zoezi zima la utoaji chanjo ndani ya Wilaya ya Ngorongoro"-Nchimbi
Bw. Nchimbi amendelea kutoa shukrani kwa uongozi mzima wa Wilaya ya Ngorongoro kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Ngorongoro kwa ushirikiano wa karibu walioutoa wakati wote wa utekelezaji wa zoezi zima la utoaji chanjo kuanzia siku ya kwanza mpaka ya siku nne
Pamoja na hayo Nchimbi amesema kuwa Divisheni ya Afya Wilaya ya Ngorongoro inatambua mchango wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kutoa magari matatu, pamoja na lita 1000 za mafuta katika kukamilisha zoezi la utoaji chanjo kwa Watoto wanaoishi tarafa ya Ngorongoro
Kulingana na takwimu Wilaya ya Ngorongoro imeshika nafasi ya kwanza katika zoezi zima la utoaji chanjo ya surua ndani ya Mkoa wa Arusha na nafasi ya nane kitaifa ambapo zoezi la utoaji chanjo Wilaya ya Ngorongoro limetekelezwa kwa asilimia 136
Aidha Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imetoa shukrani na kuwapongeza Wananchi kwa ushiriano waliyoutoa wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hili, pia imeipongeza Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Dkt. Revocatus Ndyekobora kupitia Divisheni ya Afya na Wahudumu wote wa Afya kwa kufanikisha zoezi zima la utoaji chanjo kwa mafanikio
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.