Wanafunzi wa Malihai Club shule za sekondari Wilayani Ngorongoro watakiwa kushiriki katika swala la uhifadhi maliasili na utunzaji mazingira.Hayo yameelezwa na Katibu Tarafa ya Loliondo Ndg.William Ndossi wakati wa ufunguzi wa kongamano la Malihai Club.Aidha kongomano hilo linalolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kuhifadhi maliasili na utunzaji mazingira limefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 09-11.06.2019 ambapo jumla ya wanafunzi 120 walimu walezi wa vikundi walipatiwa mafunzo. Ndosi Amesema kunafaida nyingi zinatokana na utunzaji mazingira hivyo amewataka wanafunzi kufuatilia mafunzo hayo kwa makini ili waweze kupata kile kichokusudiwa. Aidha mafunzo hayo yamefanyika katika shule ya Sekondari Loliondo yakishirikisha shule za Sekondari Emanyatha,Digodigo,Embarway,Loliondo,Nainokanoka,Arash Lake Natron,Sale,Soitsambu na yamefadhiliwa na Frankfoot Zoological Society
Bwana William Ndosi Katibu tarafa ya Loliondo(Mgeni Rasmi) akifungua Mafunzo kwenye Kongamano la Malihai Club Wilaya ya Ngorongoro lililofanyika Tarehe 9.6.2019
Vijana wa Malihai Club waionesha vitu walivyotengeneza kupitia mazingira wanamoishi
Picha ya Pamoja ya Mgeni rasmi pamoja na Waalimu walezi wa Malihai Club wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.