Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba (Mb) alifanya ziara Wilayani tarehe 28 na 29 mwezi Machi 2017. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri aliweza kutembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) katika Tarafa ya Ngorongoro na Ziwa Natron katika Tarafa ya Sale. Ziara hiyo ilikuwa na malengo yafuatayo:-
Akiwa katika Tarafa ya Ngorongoro, Mheshimiwa Waziri alitoa maagizo yafuatayo:-
Akiwa katika Tarafa ya Sale ambalo ni eneo la Ziwa Natron, maarufu kwa mazalia ya flamingo ‘Laser Flamingo’, uwepo wa madini aina ya magadi soda, uwepo wa chemchem ya maji moto na pia ni sehemu ya miongoni mwa Milima ya volcano hai ya Oldonyo Lengai.
Mheshimiwa Waziri aliweza kukagua shughuli za utunzaji na uhifadhi wa mazingira. Mheshimiwa Waziri alipokea taarifa fupi ya shughuli za utunzaji wa mazingira iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Bwana Baltazary Victor Kaiza. Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo iliainisha changamoto mbalimbali za mazingira katika Wilaya ikiwa ni pamoja na:
Baada ya kupokea taarifa, Mheshimiwa Waziri alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Wilaya katika kuhakikisha kuwa shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira zinapewa kipaumbele kikubwa. Aidha Mheshimiwa Waziri aliweza kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Engaresero kupitia Mkutano wa hadhara. Mheshimiwa Waziri alisisitiza shughuli za utunzaji wa mazingira na maliasili kwa ujumla na kuona uwepo wa Mpango wa serikali kuandaa mradi wa kulinda na kuhifadhi Ziwa Natron. Mradi huo utahusisha maslahi mapana ya wananchi waishio pembezoni mwa ziwa hasa kwa kutumia rasilimali zipatikanazo katika ziwa hilo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.