ZIARA YA MH.WILLIAM T. OLENASHA (MB)NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKINOLOJIA KATA YA OLOLOSOKWAN NA SOITSAMBU
Katika ziara yake siku ya pili allitembelea shule ya sekondari soitsambu, shule ya msingi Ololosokwani, shule ya sekondari Emanyata na kuhitimisha na mkutano mkubwa katika kujiji cha Soitsambu
Kuzindua
Alizindua miradi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Soitsambu, mradi wa bweni katika shule ya msingi Ololosokwani nyumba moja ya 6 in one inayojengwa katika zahanati ya Ololosokwan kugawa vyeti katika mahafali ya 18 ya Emanyata sekondari na kuhitimisha ziara yake katika kijiji cha Soitsambu
Aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na wale wa kidato cha nne wasibweteke kwani ni mwanzo tu hivyo wapambane kujiendeleza zaidi.
Ahadi
Katika shule ya sekondari Soitsambu aliahidi nyumba moja ya 6 in one na Olosokwani shule ya msingi aliahidi bweni la wavulana litakalokuwa na uwezo wa kulala wanafunzi 80 ambapo aliwataka wazazi wa kijiji cha Ololosokwan wachangie asilimia ishirini (20%), katika zahanati ya Ololosokwan kwenye ujenzi wa nyumba ya watumishi inayojengwa 6 in one aliahidi million 15 ambazo atazitoa katika awamu mbili.
Akihitimisha katika kijiji cha Soitsambu aliwataka wananchi kujitolea katika kufanya shughuli za maendeleo
Katika shule ya Sekondari Soitisambu Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia akimbatana na viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi akifungua jengo la darasa
Akiwa katika picha ya Pamoja na waalimu wa shule ya sekondari Soitsambu
Katika shule ya msingi Ololosokwan Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia alifurahi kwa kuimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Ololosokwan
Katika zahanati ya Ololosokwan Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba ya watumishi 6 in 1
Mh Yanick Ndoinyo akizungumza jambo na Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia alipowasili katika kata ya Ololosokwan
Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne shule ya Sekondari Emanyata
Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia akifungua jengo la bweni la wasichana katika shule ya msingi Ololosokwan
Katika kata ya Ololosokwan Mh.William Tate Olenasha (MB)Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Tekinolojia akizungumza na wananchi wa kata ya Ololosokwan
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.