Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Mohammed Bayo leo tarehe 28 Aprili, 2025 ameambatana na timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo Tarafa ya Ngorongoro.
Katika ziara hiyo ametembelea shule ya msingi Olpiro na Zahanati ya Olpiro kata ya Eyasi ikiwa lengo nikujua hali ya maendeleo katika taasisi hizo na kujionea Hali ya uboreshaji ulifanyika kwani serikali ilitoa kiasi milioni 124 za awali za kufanyia maboresho ya miundo mbinu katika tarafa hiyo huku shule ya Olpiro ilitengewa kiasi Cha milioni sita kama kiasi cha awali.
Aidha, Mhe. Bayo ametumia nafasi hiyo kujibu changamoto ya mwalimu mkuu wa shule hiyo ndugu Benjamen Ngowi ambaye alieleza changamoto ya bweni kwa kueleza kuwa Halmashauri ilishapendekeza bajeti katika Mwaka mpya wa fedha juu ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kwa tarafa ya Ngorongoro.
"Sisi kama Halmashauri tulishaandaa mapendekezo ya bajeti na pindi itakapopitishwa basi bweni hilo litajengwa katika shule hii, na Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na anawapenda Wananchi wake, pia nitoe Rai kwenu walimu muongeze ufanisi katika ufundishaji ili hali ya ufaulu wa kitaaluma uendelee kuongezeka" amesema Mhe. Bayo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.