Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel amefanya Ziara Ya Siku Moja Katika Wilaya ya Ngorongoro. Prof.Elisante Ole Gabriel alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,viongozi wa chama cha mapinduzi na Serikali katika ukumbi wa makao makuu ya NCAA. na baadae alizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mokilali katika mkutano wa Hadhara na alipaya nafasi ya kusikiliza Kero mbali mbali za Wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani waliokuwa wakimsubiria kwa shauku kubwa.
Prof.Elisante Ole Gabriel aliwaahidi wananchi hao kuwa yeye kama Mtemdaji Mkuu wa Wizara amezisikia na Anakwenda Kuzifanyia Kazi na Kuwaahidi Wananchi wa Misigiyo kuwa Serikali ya awamu ya Tano imawapenda sana Wafugaji
Katika Ziara Hiyo Pro Ole Gabriel aliambatana na Magebe Makoye ambaye ni katibu wa chama cha wafugaji wafugaji Tanzania na kuwataka wananchi ambao haswa wafugaji wa Ngorongoro kuomba kugombea nafasi mbalimbali za chama hicho kwani uchaguzi ni mwezi Nov 2018 ili wawe wateteze wa wafugaji wenzao
Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro wakiwa katika ofisi za NCAA wakimsubiri kumpoke Prof.Elisante Ole Gabriel
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rahid Taka wakimpokea na kusalimiana Prof.Elisante Ole Gabriel
Katika picha ya pamoja na Ndugu Shimba katibu wa CCM wilaya ya Ngorongoro na Mwenyekiti wa wazazi CCM ndugu A.Karanjai
Dr.Chobi Chubwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi katika wilaya ya Ngorongoro akisoma taarifa fupi mbele ya Prof.Elisante Ole Gabriel Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifungo na Uvuvi
Mh Shutuk na Mh Siloma wakiwa katika picha ya pamoja
Dr.Chobi akikabidhi Taarifa kwa Prof.Elisante Ole Gabriel Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifungo na Uvuvi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Ndugu Raphael Siumbu akiwasalimia wananchi wa Misigiyo
Mh.Rashid Taka Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro akisalimiana na Mbunge Mstaafu Ole Telele katika kijiji cha Misigiyo
Viongozi mbalimbali wakivishwa zawadi na wananchi wa kijiji cha Laitole Wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.