Mnamo tarehe 25 hadi 27 Oktoba 2017 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla alifanya ziara katika Wilaya ya Ngorongoro akiambatana na Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa William Tate Ole Nasha. Mheshimiwa waziri katika tarafa ya Ngorongoro alifanya mkutano na menjimenti ya NCAA na baraza la wafugaji. Akiwa katika tarafa ya Loliondo tarehe 26.10.2017 mheshimiwa waziri alianzia ziara katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo alipokea taarifa ya wilaya. Pia Mheshimiwa waziri alipokea taarifa za kiutendaji katika ukumbi wa Halmashauri iliyosomwa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri Mheshimiwa Emanuel Ole Shangai. Mheshimiwa Waziri alipata fursa ya kuhutubia wananchi katika viwanja vya wasso.
Mheshimiwa waziri akiwa katika viwanja vya wasso alipata kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusu masuala ya Maliasili na Utalii na kuahidi kuzifanyia kazi. Aidha Mheshimiwa Waziri alitoa tamko la kutaka kusitishwa kwa operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori tengefu la Loliondo na kutaka mifugo yote inayoshikiliwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa. Dk Kigwangalla amesema amechukua uamuzi huo ili kusimamia dhana na uhifadhi endelevu na shirikishi na kusema kuwa Wizara hiyo itaendelea kusimamia sheria za uhifadhi kwa kushirikiana na jamii na haitakubali watu wachache kuvunja sheria za uhifadhi.
Mheshimiwa Waziri pia aliagiza wataalam wa Maji katika Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na wahifadhi na Serikali za vijiji kuangalia vyanzo vya maji nje ya hifadhi ili mifugo ya wananchi ipate maji.
Akizungumzia mifugo mingine ya wananchi, iliyokamatwa maeneo mengine ya Hifadhi Nchini, Mheshimiwa Waziri aliagiza Mamlaka zote zilizo chini ya Wizara hiyo zitafakari upya namna ya kutoa adhabu na ndani ya siku saba apewe mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya mifugo iliyokamatwa kwenye maeneo mbalimbli ya Nchi ili aweze kutoa uamuzi unaofanana na aliotoa hapa Ngorongoro. Aidha waziri alisema mifugo yote katika wilaya zote za Tanzania iwekewe alama maalumu kama sheria ya mifugo ya mwaka 2010 inavyoelekeza…. “Tunataka tuitambue mifugo yote ya watanzania kwa kuiwekea alama maalum ili mifugo ikiingia kwenye maeneo tuliyoyahifadhi kisheria kutoka nchi nyingine tuitaifishe bila kigugumizi chochote”, alisema.
Mheshimiwa Waziri amesema anataka Mamlaka ambazo zipo chini yake, kurejea katika kazi ya msingi kuhifadhi na kupambana na ujangili badala ya kufanya kazi ya kuchunga mifugo inayokamatwa kwani uchukuaji mifugo inawafilisi wananchi na inajenga uadui baina ya wahifadhi na wananchi.
Aidha baada ya kutembelea eneo la ololosokwani siku ya tarehe 27.10.2017 alikagua mpaka wa hifadhi na kujionea vigingi vya mpaka (beacon) vilivyoharibiwa na wananchi.
Mheshimiwa waziri alielezwa kuwa wananchi Wanavunja beacon na nyingine zimechimbwa na kuondolewa kabisa ili kusiwe na alama yoyote. Aidha Mhifadhi alimweleza Waziri kuwa inawezekana kurudishia beacon japo ni gharama kubwa kwani hata zile zilizong’olewa kabisa alama zake ziko kwenye GPS.
Akihutubia wananchi katika kijiji cha ololosokwani Mheshimiwa Waziri alisema hatatoa jibu lolote juu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi kwani suala hilo liko katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha aliwaomba wananchi hasa vijana wakae na viongozi wayatatue matatizo yaliyopo. Waziri pia alisisitiza juu ya ufugaji wa ng’ombe wachache wenye tija kwani bila kuvuna ng’ombe malisho hayatatosha.
Akihutubia katika ukumbi wa Halmashauri wakati wa kuhitimisha ziara yake katika Tarafa ya Loliondo, Waziri kigwangala alisema amejionea mambo mengi yakiwemo maboma ambayo yako Serengeti japo ni machache lakini ndio safari ya kuingia ndani.
Waziri aliwagiza madiwani waunde kamati ambayo mwenyekiti wake atakuwa mkuu wa wilaya na wachague makamu mwenyekiti miongoni mwao waanze kuainisha changamoto moja baada ya nyingine zinazowakabili kwasababu hata kama mapendekezo yao yatapitishwa yote na Waziri Mkuu bado watatakiwa kukaa chini na kuweka utaratibu wa namna ya kuyatekeleza kwani inawezekana yakaja na utaratibu wa kufuata na kulazimu watumishi wa Serikali kufanya mambo kadhaa ili maelekezo hayo yawe endelevu na yaweze kutekelezeka.
Pia waziri alisema madiwani na jamii kwa ujumla wanatakiwa washirikiane na wataalam na Serikali kuhakikisha mpaka wa Serengeti unapimwa na usiharibiwe tena. Sambamba na hilo wahakikishe panatengenezwa utaratibu wa matumizi bora ya ardhi ambao ni shirikishi ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili.
Waziri pia alisema atatuma wataalam wake waje kufanya tathmini ili watoe ripoti ya namna wanavyoweza kuja kuwekeza katika malisho ya mifugo, elimu ya ufugaji bora wa kisasa, mbegu bora ya mifugo na ya kisasa na maji. pia atawaagiza Mamlaka zilizopo chini ya wizara yake kuja kutathmini namna ya kuanzisha soko la mifugo na kutoa elimu ya kuwawezesha namna bora ya kuanza kuvuna mifugo.
Hata hivyo Naibu Waziri wa Elimu Mheshimiwa William Ole Nasha alivitaka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vichukue jukumu la kuchunguza ili kubaini kama kuna wakenya katika eneo la mgogoro au la na endapo wakibainika hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.
Waziri kigwangala alihitimisha kwa kusisitiza yafuatayo;
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.